
<tc>Cocoa Butter (Mafuta ya Cocoa Butter)</tc>
Mafuta ya Cocoa Butter: Unyevu wa Asili kwa Ngozi Laini na Nywele Zenye Afya
Jina la Kisayansi:
Theobroma cacao
Maelezo:
- Cocoa Butter ni mafuta mazito ya asili yanayotolewa kutoka kwa mbegu za kakao nchini Ghana.
- Yana utajiri wa mafuta ya asili (fatty acids), antioxidants, na vitamini E ambayo husaidia kulainisha ngozi, kuongeza unyumbufu wa ngozi, na kutibu ngozi kavu au iliyoharibika.
- Yana harufu laini ya chokoleti na muundo laini, ndiyo maana hutumika sana kutengeneza body butters, balms na bidhaa za nywele.
Aina ya Bidhaa:
Mafuta magumu (huyeyuka yakigusa ngozi)
Viambato:
Cocoa Butter safi 100% (Theobroma cacao)
Faida na Matumizi:
Kwa Ngozi:
Hunyunyiza na kulainisha ngozi kavu, ngumu au iliyopasuka
Huboresha mwonekano na unyumbufu wa ngozi
Hupunguza muwasho na kusaidia ngozi nyeti au yenye eczema
Kwa Nywele:
Hufunga unyevu na kulinda dhidi ya ukavu
Hulainisha nywele na kupunguza kufrizz.
Namna ya Kutumia (Matumizi ya Nje Pekee):
Kutumia Moja kwa Moja:
Pasha kiasi kidogo kwa mikono na paka kwenye ngozi au nywele.
Kutengeneza Body Butter / Balm:
Yeyusha na changanya na mafuta kama nazi, almond au jojoba
Huduma ya Midomo & Kucha:
Tumia kidogo kulainisha midomo kavu au kupaka kwenye ngozi ya kucha
Kuzuia Stretch Marks:
Sugua kwenye maeneo yenye alama kila siku wakati na baada ya ujauzito.
Tahadhari:
Kwa matumizi ya nje pekee
Fanya jaribio kwenye sehemu ndogo kabla ya kutumia kwa ngozi nyeti
Epuka kuingia machoni na sehemu laini za mwili
Uhifadhi:
Hifadhi sehemu kavu, baridi na mbali na joto kali
Funga vizuri ili kudumisha ubora na harufu yake